55 ONYA WATU! UHARIBIFU [MKUBWA] WAJA!!!

print
UNABII 55

ONYA WATU! UHARIBIFU [MKUBWA] WAJA!!!

 

UMEANDIKWA/ UMESEMWA CHINI YA UPAKO WA RUACH HA KODESH KUPITIA MTUME ELISABETH SHERRIE ELIJAH (ELISHEVA ELIYAHU)

[Huu unabii mpya kutoka kwa YAHUSHUA unajumuisha masomo katika kutafuta Bwana kwa bidii, ndoto Anayoitia Mitume na Manabii WAKE kuisoma na kuiagua, kutoruhusu kuzima upako, na onyo kali kwa wale ambao Anaita kusaidia hii huduma na wanapuuza Sauti YAKE.]

*******

Hii inatoka Unabii 105, YAHUVEH Alisema ujumbe huu uwekwe katika kila Unabii kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisheva(Elisheva) kutoita Huduma baada ya jina la mwanaume au mwanamke hata kabla kuwepo na huduma. Niliweka ndani ya roho yako kwa kuwa hakuna lolote kwa haya ambalo limefanyika kwa mkono wako, hakuna lolote kwa haya ambalo limetoka kwenye kinywa chako. Limetoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH ambaYE amezaa. Limetoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako ambaYE amezaa. Limetoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako ambaYE amezaa. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa upepo wa SH’KHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, Upepo Takatifu wa Uamsho, sio kwa pumzi yako au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Julai 2010 MUNGU YAHUVEH pia alisema yaongezwe haya kutoka Mambo ya Nyakati ya 2 kabla ya kila Unabii:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

*******

 

[Watoto] WANGU wapendwa, huwa mnaNIkumbusha kuwa MIMI huadhibu na kukemea wale ambao NInapenda. Lakini Mpendwa WANGU, hujui kuwa MIMI pia NInatuza kwa bidii wale wanaoNItafuta. Una bidii, masaa 24 kwa siku, hata katika usingizi wako, kwa bidii unaNItafuta. Je! Vipi NAweza zaidi watuza Watoto WANGU ambao wanajitahidi kutafuta kila neno LANGU?

Uharibifu unakuja. Kuweni tayari. Uharibifu unakuja. Hiyo ndiyo sababu Ninamwambia Binti YANGU sasa; iseme katika neno lililosemwa. Haiko pekee katika nguvu za neno lililoandikwa. Miaka mingi iliyopita NIliamuru haya maneno yasemwe, na bado NIlijua wale mameneja wa tovuti [waliokuwa] hawangetii. Ingawa, sasa ndio wakati. Haya maneno ya kinabii yanasemwa. Kila siku [unabii] mpya utaongezwa. Zote zitakuwa pale ambapo zitasikika, sio tu kusomwa.

Uharibifu unakuja. Tafuta hiyo ndoto, ile ya mwisho ambayo NIlimpa Binti YANGU. Uharibifu unakuja. Tia lebo hii. Onya watu. Waambie NInatuma Mitume na Manabii WANGU kuonya watu kabla uharibifu uje. Uharibifu unakuja lakini sio kwa Watoto WANGU, sio kwa Bibi arusi WANGU, sio kwa wale WANGU Waliochaguliwa na sio kwa wale Wateule WANGU, NInaenda kuwalinda kama vile Nuhu na familia yake walilindwa katika safina, ikiwa tu wanaweza kuamini. Waambie, NItawalinda kutokana na mafuriko ya uovu. NItawalinda kutokana na mafuriko ya hatari zinazongojea.

Waambie, “Ingieni kwenye Safina.” Wapate kujua pale wanapopaswa kuwa. Waambie watafute uso WANGU. Ikiwa hawajui pale wanapofaa kuwa, wafunge na kuomba na kulia na kuomboleza lakini wajue pale safina yao ipo. Mradi wanatambua pale wanapaswa kuwa, mradi wako chini ya mwavuli WANGU wa Usalama, basi wamo ndani ya safina, haijalishi walikomo duniani. Lakini NAwaambieni tena, Watoto WANGU, iteni Mitume na Manabii waague ndoto NIliyompa Elisheva. UHARIBIFU UNAKUJA.

Lazima muweke [kwenye tovuti] ile ndoto na NItawapa aguzi moja ya hiyo ndoto. Lakini iteni Mitume, na iteni Manabii, kwa maana kila mmoja atakuwa na sehemu ikiwa tu watatii na watawaeleza ufunuo kamili wa hiyo ndoto. Kwa Watoto WANGU wapagani wanaleta uharibifu na NInairuhusu. Lakini wale wanaoNIlilia, katika Jina la MWANANGU YAHUSHUA, watakuwa katika safina ya usalama WANGU, NItawakinga kutokana na uharibifu na uchungu. Katika herufi kubwa, wekeni hii tarehe na saa chini pamoja na ndoto na mwaambie, kama vile katika siku za Nuhu, kama vile katika siku za Lutu.

UHARIBIFU UNAKUJA!!!

Hamjui ni saa gani. Hamjui ni siku gani. Lakini katika siku ya Sabato. [Simu inasikika inalia katika usuli.] Ni bora uwe katika maombi! Ujumbe wa Uharibifu – Katizo Huzima Upako – Onyo [Elisheva amekengeushwa na kulia kwa simu, anaendelea kuomba katika ndimi.] Na pale imani yako ipo, usalama wako utakuwa. Usalama wako hauko. [Ujumbe unasikika ukiachwa kwenye mashine ya kujibu.] Adhabu Kwa Kuruhusu Upako Kuzimwa wakati Mwingine, Watoto WANGU, jifunze somo. Chomoa hiyo simu. Musiwahi tena acha nafasi upako unaweza zimwa. [Elisheva anaendelea kuomba katika ndimi, aking’ang’ana kuregesha mawazo yake kwa yale YAHUSHUA Anamzungumzia.]

Hii inaNIkasirisha. Wakati mwingine mjihadhari. Ndungu ***** hakujua. Hakuelewa alicheza katika mikono ya shetani. NInakusamehe, lakini hili ni somo jingine jinsi ni rahisi upako unaweza kuzimwa na kikengeusha-fikira tu. Hiyo ndio maana NInakuamrisha uwe katika faragha, Elisheva, panapo na vikengeusha-fikira vichache iwezekanavyo. Kwa maana unakaa katika upako zaidi na kingeusha-fikira chochote kinaweza uzima. Niliruhusu haya yatokee wakati binti YANGU alikuwa akisema maneno kutoka KWANGU ili kuwaonyesha jinsi ni rahisi mnaweza kengeushwa na mkose kusikia kutoka KWANGU tena. UHARIBIFU UNAKUJA!!!

Onya watu tu kwamba Uharibifu unakuja.

Onyo Kali Kutoka YAHUSHUA: “Je, Unasikia kutoka KWANGU kusaidia hii Huduma na unapuuza NInachokuambia ufanye?” Chochote wanachoenda kuNIfanyia, chochote wameahidi wanaenda kuNIfanyia, je, NImeiweka kwenye moyo wao kusaidia hii huduma? Je, wameiairisha na kusema, “Ee kesho ama labda siku nyingine. Nitakuja tu na nitasoma tu, sita hata wasiliana nao.” Wanavyo vipaji na bado wanachagua kutoshiriki kwa sababu wanasema, “Ee katika siku nyingine.” Lakini NInawaambia hili, na NInaisema.

UHARIBIFU UNAKUJA!!!

Na chochote wameNIfanyia, chochote wamefanya katika JINA la MWANANGU; kwa namna yoyote wamesaidia Habari Njema kuenezwa, hawa ndio NItakaosikiza vilio vyao. Sadaka zozote wamezitoa, NItazingatia katika siku hiyo. NItazingatia nani waliofunika masikio. NItazingatia nani waliofunika macho yao. NItazingatia wanapoona ukiwa na uhitaji, na hata NInapoiweka kwenye moyo wao, ungana mikono na muwe waaminifu na wale wanaoeneza mbegu YANGU nzuri kwenye shamba la mavuno, na wanatikisa vichwa vyao na kukana na kusema, “La hasha, HAniongeleshi. NAwaonya sasa, NItazingatia. Kwa maana NInamtuma kama Eliya wa Zama(katika Kiebrania, Eliyahu). NInamtuma kwa wajane wa Sarefati, ingawa hawakujua. NItazingatia siku uharibifu utakuja.

Je, walisaidia kulisha Manabii WANGU? Je, walitoa maji? Je, walitoa neno la kutia moyo? Je, walitoa makazi? NInawauliza manabii wa zama tena na tena katika Neno ambalo limetabiriwa na siku zote NIliwatuma na Ujumbe WANGU na ilikuwa wakati wote chaguo lao ikiwa watu watasikia au ikiwa wataitikia katika hofu ya kimungu ama kama wangewafukuza manabii? Hakuna kilichobadilika leo hii.

Kwa hivyo waambie, Binti YANGU, waambie kwa niaba YANGU ili wasiseme hawakuonywa.

UHARIBIFU UNAKUJA!!!

Je, wako tayari? Waulize nini wameNIfanyia MIMI!

Mwisho wa Unabii

 

*******

 

Unabii 55 – Ndoto

YAHUSHUA! Sisi Ni Bi-arusi Wako! Tunakungojea!

Muhimu, ndoto ya hivi karibuni ni maombi pekee yake yanawezazuia hii kutendeka, maaguzi yapo chini ya huu ukurasa. Tafadhali nisaidieni kupiga baragumu [shofar] ya onyo. Ikiwa wachungaji wenu hawatasikiza, basi mnawajibika kuongea hata hivyo. Nina uharaka katika roho yangu. Nilikuwa na ndoto wazi mnamo Des. 19, 2001. Sababu ya pekee nawashirikisha sio kufanya hofu, lakini badala yake kuwauliza maombi yenu kwamba hii ndoto isije ikatimia. YAHUVEH Anaongea nasi katika maono, ndoto na mafunuo pia katika unabii. Ni maombi ya bidii ya watu wema pekee yatasimamisha hii ndoto kuwa jinamizi. Tafadhali shiriki hii na wengine, na uliza kanisa yenu waanguke kwa nyuso zao na kutubu na kuuliza rehema juu ya Marekani mara nyingine. Kama makanisa au wachungaji watakataa, basi anzeni maombi ya makundi na muombe.

Hii ni muhimu. Naishi Marekani. Je, nawezaje kosa kujali? Je, hii ni Marekani naona? Nchi itapigwa mara mbili wakati usiotarajiwa. Tuna ulinzi wa jeshi la nguvu lakini YAHUVEH pekee ataweza kusimamisha au kuzuia kile shetani anataka kufanya na ni maombi ya bidii pekee ya watu wema ambayo yatazuia au kuisimamisha! Lazima tujali. Ni wangapi wasiokoka ambao unajua?

 

*******

 

Ndoto [iliyo] na Mtoto Mchanga aliye na Njaa

Nilikuwa nimesimama nje nikiangalia anga nzuri ya bluu, kote kulikuwa na amani. Nilipokuwa nikiangalia juu niliona miviringo 4 angani ikichorwa ni kama kidole cha Mungu YAHUVEH kilikuwa kinaichora polepole. Mviringo wa nne ulipochorwa, nilisikia kelele ya mgurumo mkubwa, nikaingia ndani ya nyumba, upepo MKUBWA ulikuja ukiharibu na kuuwa ilikuwa ni kama mlipuko wa nyuklia kutokana na athari za bomu ya nyuklia! Niliangalia katika hofu yale maafa na uharibifu. Katika nyumba yangu niliona mwanamke na kitoto kidogo mikononi mwake. Nilikiangalia na kitoto kilionekana kama kimekufa na kuwa utapiamlo sana. Nikasema, “Mbona hukumlisha mtoto?” Aliniangalia kwa ubaridi na kusema “Kwa sababu mtoto amefunga.”

Halafu kabla nikichukue kitoto kutoka kwake, alifungua dirisha na kukitupa nje [kutoka] dirisha la ghorofa ya pili. Nilikimbia nje katika ule mnururisho na upepo wa kuharibu, na kukishika kitoto mikononi mwangu, na kikaanza kupumua tena! Nilipokuwa nimesamama pale mwanaume alikuja kwangu uso wake ulikuwa umechomwa vibaya sana kutokana na mnururisho, na ulikuwa mwekundu na kiwango cha tatu cha kuchomwa, hakusema kamwe neno moja, alitembea na kunipita tu. Nilirudi ndani ya nyumba yangu, nikiwa nimelindwa kabisa kutokana na mnururisho, na nilijua hakuna chochote kingeniumiza pamoja na kitoto na nikakilisha maziwa kutoka kwenye chupa.

Baada ya muda zile upepo za kuharibu zilisimama. Yote ilionekana kuwa na amani. Halafu nikaangalia anga tena, na nikaona mviringo wa kwanza ukianza, nilianza kupaaza sauti Tubuni na mgeuzie mioyo yenu YAHUSHUA kwa maana tena hukumu imekuja. Wachache saana walisikiza! Niliona ile miviringo nyingine mitatu yote katika safu, 4 kwa jumla, na kisha sauti ya mgurumo ambao siwezi kueleza. Halafu ule upepo wa kuharibu ukaja tena, kana kwamba mlipuko wa nyukilia mwingine ulitokea. Nilifahamu yule mwanamke ni dini, na kitoto ni mikusanyiko ya waumini, dini ya utaratibu inakosesha watu chakula cha kiroho ikiwalazimisha wafunge kwa ajili ya maarifa zaidi ya kiroho na ukweli za kinabii na mafunuo. Ninatumiwa kulisha watu ambao wamekoseshwa [chakula cha kiroho] katika kanisa zao, wachungaji wanatoa dhabihu watu kwa ajili ya kujilisha utajiri, udhibiti, wakifikiri wao wanamiliki kondoo, wakisahau kuwa kuna Mchungaji Mzuri mmoja pekee.

Tafadhali onya kila mtu. YAHUVEH aliniongelesha katika hiyo ndoto na kunionya kwa nini atainua ua lake la ulinzi tena, hata wapagani wanaabudu mungu wa kipagani, na ni nani Marekani wanamwabudu?

*******

Katika Novemba nilikuwa na ndoto kama hiyo.

Nilikuwa nikitembea kwenye barabara na ng’ombe iliyojaa maziwa ilinifuata popote nilienda. Haikuwa ng’ombe yangu. Mkulima alinishtaki kwa kumuibia ng’ombe yake. Nilisema singeweza kufanya ng’ombe iache kunifuata; ilikuwa ni chaguo lake. Niliona miraba 3 katika mstari ikichorwa na kidole cha YAHUVEH katika anga. Nilisikia sauti kama mgurumo. Siwezi ieleza. Halafu niliona niko kwenye milima na mawe makubwa yalikuwa yanaelekea kule nilikuwa. Nilikimbilia bahari kule nyumba yangu ilikuwa kwenye ndoto. Niliingia katika nyumba. Halafu nikaona hizo miraba 3 tena ikiwa inachorwa katika anga. Niliangalia katika hofu, na nilijaribu kufikiria, ni njia ipi ya kufa ilikuwa isio na uchungu kabisa, kwa maana nilidhani bahari ingefunika nyumba na wote wangezama majini kama ningebaki kwa hivyo niliamua kuenda kwenye milima tena. Nilisikia ule mgurumo na punde mraba wa 3 ulichorwa niliona kabla ningeweza kusonga fataki angani, kwanza eupe ya kupekecha, halafu fataki za rangi zenye kung’aa. Ilikuwa fataki za kupendeza. Sikukimbia, niliziangalia tu zile fataki.

Tafadhali nitumieni ufahamu wenu wa hizo ndoto. Najua hiyo ng’ombe ni watu waliojaa maziwa kutoka kwa mafunzo ya wachungaji wengine, lakini wanataka zaidi. Ni sala za bidii za watu wema pekee zitakazo leta mengi, kama watu WANGU wataanguka kwenye nyuso zao na kunyenyekea, NItasikia maombi yao na kuponya nchi yao! Tafadhali chukueni hizi ndoto kwa uzito. YAHUVEH Aliniongelesha kwa sauti miaka 3 iliyopita na 2003 utakuwa mwaka wa nne. Alisema, “Katika misimu mine utajua.” Tukifahamu vizuri, hiyo misimu minne ni miaka. Je, tuna huo muda wote au mwisho utakuja kabla yake? Kwa maana wengi zaidi wana tamanio la kuangamiza Marekani na wana hizo nguvu na YAHUVEH na YAHUSHUA pekee YAO WAnaweza ikomesha. Atatumia maombi yetu. Ni nani atatusaidia kuomba? Lazima tuwe na muda zaidi wa kufikia hii dunia kwa ajili ya Ufalme wa Mbinguni.

Kitu kimoja kizuri ni kuwa nimelindwa. Pia nawe ikiwa uko chini ya mabawa ya YAHUVEH kama ilivyoelezwa katika Zaburi 91, pahali pa siri pa MUNGU AliYE Juu Kabisa. Je, kunacho kitu kigumu zaidi kwa MUNGU? Wale watoto 3 Waebrania walitupwa kwenye tanuri ya moto iliyotiwa joto mara 7 zaidi na hakuna kilichochomwa bali zile kamba zilizotumiwa kufunga mikono na ni miguu yao. MUNGU YAHUVEH Anaweza tuepusha na madhara wakati huu pia.

Tafadhali ambia wengine kuhusu wokovu wa neema ya YAHUSHUA ili waokolewe. Usiogope mwanadamu ambaye anaweza angamiza mwili pekee, lakini bali fanyia bidii wokovu wako kwa uwoga na kutetemeka na YAHUVEH AmbaYE Anaweza kuua mwili wako na kutupa roho yako katika Ziwa la Moto. Kwa sababu ninawapenda, ninawaonya. Ezek 3:17-21 damu haiko kwenye mikono yangu. Tafadhali kumbukeni siku ya Sabato ya ukweli na muiweke Takatifu. Kuishika Sabato haimaniishi usheria [ushikiliaji mno wa sheria], tahadhari usheria na utumwa, hii ni baraka na pumziko kwa watoto wa YAHUVEH. Kama vile katika siku za Musa kutakuwa na baraka za ulinzi kwa watu ambao wanaishika Sabato ya Ukweli kwa sababu ya upendo wa YAHUVEH na YAHUSHUA. Haya maagizo tulipewa na Adamu na Hawa, na Bibilia inasema Sabato ni ya milele na haitawahi badilika. Ukatoliki ulibadilisha Sabato ya ukweli; siku zote abudu lakini hasa karibia zaidi katika Sabato ya kweli. YAHUSHUA Alikuja kutimiza Sheria ya Musa, sio kuifuta. Nyumba ambayo ninakimbilia ndiyo Safina yangu ya usalama. Hakikisha uko katika Safina, hii itakapofanyika chini ya kinga ya Zaburi 91. Kumbuka ita JINA la YAHUVEH na YAHUSHUA. Kuna nguvu katika Majina Matakatifu.

Upendo na Baraka katika MAJINA ya kustaajabisha ya YAHUVEH na YAHUSHUA. Mtume Elisheva Eliyahu

 

******

Uaguzi wa Kwanza:

Mpendwa (Elisheva ),

Ninaomba kuhusu hiyo ndoto. Ninaamini ni dhahiri kwamba Bwana anakuonyesha yule kahaba na hayuko radhi kumlisha mtoto wake nyama ya Bwana. Kwa hivyo Bwana Ameazimia hukumu juu yake. Mara tatu Bwana amemwongelesha. Hukumu zinaanza kuja na zinaanza na yule Kahaba. Yeye ni yule kahaba mkubwa aliyeandikwa kuhusu ambaye amepanda yule mnyama. Mungu Amemwongelesha mara mingi zisizohesabika na ni wakati wa kutoka ndani mwake watu wangu na ili msishiriki dhambi zake. Mbona mnaendelea kuenda katika nyumba za makahaba na kushibishwa kwenye maziwa ya kiroho ambayo hayawezi wafanya mkue hadi mkomae?

Na sasa Bwana Ametuma kukonda kwa nafsi zenu na bado mnashindwa kutoka ndani mwake watu wangu. Na kwa nini? Ili muwe na marafiki wazuri na nyumba nzuri na magari mazuri na pahali pazuri pa kuabudu? Mbona mnapaswa kuwa na hivi vitu vyote na bado mnanisahau siku bila mwisho. Bwana Aliyewapenda na kuwaokoa na kuwalisha na mnaenda baada ya yule malaya na yule kahaba? Na je, atawalisha vipi oh nyinyi wajinga mnaonisahau siku bila mwisho? Mbona mmetafuta yule Kahaba na kiota chake cha mitego badala ya Bwana?

 

Kwa hivyo kwa sababu mmetafuta yule Kahaba na hamjanitafuta na hamjatii sauti yangu mtoke ndani mwake, Sitasikiza Nitakapotuma hukumu zangu dhidi yake. Hivi vitu ilipaswa msishiriki ndani. Lakini ulisema ndani mwako, “Je, kunayo njia nyingine? Kwani si njia ya yule Kahaba ndiyo njia pekee ninayoweza enda? Kwani si kuna majengo kwenye kila kona na siwezi pata nyama pale?” Lakini ulijiambia, “Kwani ni nini? Angalau nina mahali pa kuishi kando ya barabara pale wanaweza nilisha na kuninawirisha na naweza kuwa na utajiri na mafanikio pia!”

Na yule Kahaba alibembeleza na akalia pole pole na akawavuta ndani na mkakula mkate katika pahali teuzi na mkapata amani na faraja kidogo. Lakini Nilisema “Hawa watu hawataNisikiza, inabidi Nitume mwito wenye nguvu isije wakafurahia yule Kahaba saana na akawabembeza watu wangu hadi walale”. Lakini uharibifu ulipokuja Nilisema, “Angalia sasa na uone, je, atatubu je, watu wataona kuwa wanaNihitaji? Je, watatubu kwa kuishi kwa sababu yao na hizi nyumba zilizojengwa katika Jina Langu? Oh je, watasikia sasa wanapoona kuwa nyumba zao zilizojengwa katika Jina Langu haziwezi waokoa, haziwezi walinda? Je, nyumba ya saruji na tofali inaweza kulinda mpendwa Wangu? Je, watu, wachungaji wanaowauzia Jina Langu na jeshi Langu je, wataweza wasaidia wakati Nitaamrisha hukumu juu yake? Je, atakuja kwa matanga yako? Je, atakutengezea kitanda chako cha kufa? Je, ataimba kwenye mazishi yako? Ninasema hapana!”

Kwa maana Nitamhukumu asema Bwana na hukumu itakapokuja yote ambayo yanachukiza yatachomwa na moto. Kila kitabu cha nyimbo cha mwisho ambacho mliaminia. Kila mnara na kengele na kifaa cha muziki cha mwisho vitaharibiwa. Na ni kwa nini mnasema? Je, haikuwa tosha kuabudu [kila] Jumapili na kukutana Jumatano na kulipa fungu la kumi na sadaka na kupeana kwa kanisa la [nyumbani]? Kwani sikulipa Bwana haki Yake nilipoomba? Lakini haukuNijua. HaungeNijua. Haungetaka kuchukua wakati kuMjua akuokoaye. Ulitumia siku zako ukiishi katika ubatili na kiburi cha akili yako na ukasahau Yule ambaYe Anakupenda na Akakufia.

Na sasa Siwezi wavumilia tena. Siku ziko hapa ili mjue Yule Aliyewafia ni kweli. Mkitubu na mgeuke kutoka kwa dhambi zenu na muNiinamie na muNifuate mtaokolewa. Lakini Nitahukumu yule Kahaba mkubwa [Mimi] Mwenyewe na wamelaaniwa wale watakaopatikana ndani yake katika siku hiyo. (Elisheva ), sijefichwa kile Bwana Anaenda kufanya. Nimekuwa nje ya yule Kahaba miaka mingi.

(Elisheva ), sijafichwa kile Bwana Anaenda kufanya. Nimekuwa nje ya yule Kahaba miaka mingi. (Elisheva ), yule Kahaba mkubwa ndiye mfumo wa dini ya bandia ambaye anauza Yesu kwenye kona za mitaa na katika majengo makuu yaliyojengwa duniani. Wanauza Yesu kwa madola na kulisha watoto mkate, wakati wanaweza walisha zaidi. Lakini wanataka utajiri wa madola kutoka kwa watu ili walishe watoto maziwa na hayo maziwa yameendelea kukosa nguvu vile ulafi unavyozidi. Ijapokuwa wachungaji, wengi wao wanayo nyama au mambo mazito ya neno ndani mwao na katika mioyo yao hawaishiriki kwa sababu hii. Wanaogopa kuchukiza watu na kupoteza ufuasi na kupoteza pesa za kuendeleza majengo na programu na kama vile.

Hiyo ni dhambi kubwa na mvundo mkubwa kwenye mapua ya MUNGU. Jinsi inavyokuwa kwamba ni Mitume na Manabii wa ukweli pekee wanafanya kazi kujitegemea na ufuasi mdogo ilhali wafanyakazi wa kukodiwa wa uongo wa kanisa la Waasi wanajitajirisha na mali ya watoto. Na kwani haikuwa hivo katika wakati wa kwanza Yesu kuonekana? Walikuwa wakinunua na kuuza njiwa kwenye hekalu. Sasa wanauza kanda, na vitabu,na sanamu, na vitu vidogo vya thamani ndogo, na kahawa, na chakula, na kila aina ya vitu na hapo baada ya wamechukua fungu la kumi na sadaka. Je, Mungu hatahukumu kanisa kama hili? Je, Mungu ataruhusu huu uovu uendelee? La na mara elfu la!!! Sasa ghadhabu ya Bwana imewashwa dhidi ya waongo na atamtapika kutoka kwa mdomo wake.

Bado Anaita bi-arusi wa kweli kutoka katika kanisa la bandia la kahaba. Hiyo inamaanisha kama uko katika dini, toka. Kilutheri, toka. Kimethodisti, toka. Kipresbaiteria, toka. Toka katika kila kitu kinacho jiinua juu ya Bwana na kanisa la ukweli. Kwa maana dhambi zake zimefika juu mbinguni na Bwana amekumbuka dhambi zake. Na Mungu atahukumu vikuu huyu Malaya anayekaa kama malkia na anafikiri hatawahi ona huzuni. Jinsi gani anathubutu kujiinua vikuu hivyo. Anafikiria yeye ni nani hadi anamwaga na kutema na kujitangaza malkia na hatakuwa mjane! Tokeni ndani mwake watu wangu. Je, wewe ni mkatoliki? Toka! Toka! Toka! Ndio tarumbeta inalia unaweza kuisikia? Siku zimetumika vizuri. Hauwezi badilisha yule Kahaba. Yule Kahaba atakubadilisha!

Hakuna anayeweza kubadilisha yule Kahaba. Kama hiyo ingewezekana Bwana angembadilisha. Lakini sasa anajitajirisha na mali ya watoto wangu wasiolishwa chakula cha kutosha na hatawalisha hiyo mali na ufunuo wa neno langu lakini alikuwa ametenda dhambi za Yuda aliyeniuza kwa sarafu thelathini za fedha. Wacha yule ambaye ana sikio asikie kile roho anaambia makanisa. Leo ndiyo siku ya kusikia. Usiufanye moyo mgumu kama katika ile siku ya uchokozi wakati wana wa Israeli walianguka nyikani kwa sababu hawakuwa wameshibishwa na mkate wa ukweli kutoka mbiguni. Toka. Toka!!!! Asema Bwana.

*******

 

Uaguzi wa Kuongezea:

Uaguzi wangu wa ndoto huwa mwepesi sana. Natumai wengine wataweza kutambua maana ya ndani zaidi kama ipo. Uharibifu utakuja haraka, ghafla, ukichukua kila mtu (ila wale wanaoupanga) kwa mshangao kabisa. Ile miviringo 4 inarejelea yafuatayo, yaliyowekwa kwenye hii tovuti: Elisheva Eliyahu aliamka Baba YAHUVEH akisema mnamo Okt. 16 1999 yapata 7:00 asubuhi wakati wa kati…”Katika misimu mine utajua, kipaji cha kuponya sauti ya tarumbeta!” Hiyo miviringo 4 inarejelea hii Misimu Minne [Kaskazi, Masika, Kipupwe, Vuli?]. Elisheva alionyeshwa ukamilisho au mwisho wa msimu wa 4 na kile kitakachofanyika wakati huo. Kuiona tena mara ya pili inahakikisha huu ni unabii kutoka YAHUVEH ambao utakuja kutimizwa, pia kwamba kutakuwa na mawimbi mawili ya uharibifu. Sauti ya tarumbeta (shofar) itaita Biarusi wa YAHUSHUA nyumbani kwa usalama kabla uharibifu uje kwenye Karamu ya Harusi ya Mwanakondoo.

Hata hii dhoruba inapokimbia katika sehemu mbalimbali nchini, kanisa potovu zitaendelea kutapeli usharika (waumini) wao huku wakifanya waende njaa kiroho. Yule mwanamke ndiye hiyo kanisa, akitupa usharika wake wenye njaa kutoka dirisha la ghorofa ya 2. Elisheva, akiwakilisha wale wanaofunza ukweli na wanao walisha wale wanaowageukia kutafuta msaada, analisha kile kitoto kilicho na njaa. Yeye na kile kitoto walikuwa wamelindwa kikamilifu kutokana na mnururisho [radiation] katika nyumba yake kwa sababu ya uaminifu wake na utiifu kwa mwito wa YAHUSHUA.