10 CHUKUENI YOTE AMBAYO SHETANI AMEIBA!

print

UNABII WA 10

CHUKUENI YOTE AMBAYO SHETANI AMEIBA!

Imepewa kwake Mhubiri Elijah (Elisheva Eliyahu)

Disemba 4, 1997

* * * * * * *

Kutoka Unabii 105, YAHUVEH Alisema ujumbe huu uwekwe katika kila unabiii kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisheva kutoita huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke hata kabla kuwepo na huduma. Niliiweka ndani ya roho yako kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako au lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha RUACH ha KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa upepo wa SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, upepo Takatifu wa uamsho, sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Unabii Unaanza

Enyi Mashujaa Wakuu, siku moja mtasikia, “Ewe mwana mzuri na mwaminifu ingia ndani sasa na upumzike lakini kwa muda usio mrefu na Bwana Arusi wako yuaja.” Shikilieni pindo la vazi LANGU. Shikilieni na msiiachilie. Ingawa mtachoka, ni kwa sababu YANGU mnateswa. Kwa kuwa hii siyo kazi yenu, huduma yenu, lakini YANGU. Ni kwa sababu ya YAHUSHUA (YESU) mnapambana na hamfanyi kazi bila sababu. Kwa kuwa Mpendwa, mwasikiza RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu) anavyowaambia?

Hamna hata anasa moja uliyopoteza ambayo hautaipata tena ikiwa imefinywa, kutingizwa na kufurika. Je, kwani sitakupa na kufanya binadamu wakupe na kuhamasisha yale ambayo ni YANGU na sio ya kwako? Kwa kuwa mali yako sio ya dunia hii, lakini kwa dunia inayokuja, Ndivyo Asemavyo YAHUVEH. Mali yako Mpendwa WANGU imehifadhiwa kwako kule Mbinguni. Mali yako ni nafsi uliowaleta KWANGU MIMI. Mali yako ndiyo zawadi Nilizokupa wewe bure. Mali yako ni wale mashujaa wakuu wa maombi wanaokulinda na kukuunga mkono kwa maombi yao. Mali yako ni uwezo wa kusikia sauti YANGU kwa unyofu. Mali yako ni kujua kuwa umezungukwa na wingu la mashahidi na wanatazama yote unayofanya na kusema, ni kwa Utukufu WANGU na kwa sababu YANGU umekuwa bila.

Umejua mateso tele, lakini jua haya, maadui watakaojitokeza dhidi yako sijawatuma na sijazungumza kupitia kwao. Usidanganyike, kama hawakuinui, wanakuweka chini. Kama wale wanaosema kuwa wao ni marafiki wako na kumbe hawaungani nawei katika maneno madogo, hawatakuwa waaminifu katika maneno makubwa, jihadharini kwa kuwa sio wote wanaoniita Bwana ni Mtoto au mtumishi WANGU. Sio wote wanaosema rafiki ni rafiki wako.

Kwa hivyo Nasema kwako, “Umezungukwa na wale wanaosema, ‘Lakini mimi ni rafiki yako,” na kumbe hawajui neno rafiki na uaminifu ni nini. Wao ni Yuda waliotumwa kukusaliti, lakini Nakuonya sasa kupitia dada yenu, huyu Nabii, ili mjihadhari. Wao wana sababu zao: mipango yao ya kujikuza wao wenyewe. Jihadharini kwa kuwa mtaona vizuri sasa yale ambayo hamkuweza kuona vizuri hapo awali. Mmepewa karama mpya leo hii na Ninaizumgumza sasa kupitia huyu dada yenu, chombo CHANGU kilichojawa na RUACH ha KODESH WANGU.

Atakachozungumza itakuja kufanyika mnavyosoma barua hii iliyotumwa kwako kutoka kwa MUNGU. Mpendwa WANGU Ninakupa upako mpya ili uweze kuona ndani kwenye kina za nafsi za binadamu. Utajua karama kuu ya utambuzi kushinda hapo awali. Lakini hautapenda utakachoona, kwa kuwa kunakuja wale uliofikiria unaweza kuwaamini na utapata kuwa hauwezi kuwaamini kabisa. Wao ni Yuda waliojificha. Jihadhari kwa kuwa watafanya chochote ili kuona uovu ukikuangukia. Lakini Nakuambia utakapoona haya, wakemee katika JINA LANGU, na utaona maadui wakikimbia katika pande saba. Watakimbia kujificha kwa kuwa Ninakupa leo hii karama kuu ya ujasiri.

Kwa kuwa MIMI sio MUNGU Mkuu wa upendo tu, lakini wa vita pia na Nimekadiri vita kwa maadui WANGU. Nitakutumia kuwakemea watu watakaojitokeza dhidi YANGU na yote yaliyo Takatifu. Maneno haya sio na hayatakuwa maneno yako, kwa kuwa utajua wakati wa kuzungumza, na wakati wa kunyamaza. Utaendelea kuwakusanya Watoto WANGU pamoja, ukichukua yote adui aliyoiba, na kuwaleta mbele YANGU.

Wewe ni dhabihu iliyo hai KWANGU MIMI. Kazi unayoifanya haifanywi katika nguvu na uwezo wako, lakini katika nguvu na uwezo WANGU. Ingawa wewe huchoka nyakati nyingi, kumbuka kuitisha nguvu YANGU, ujasiri WANGU. Kumbuka kuitisha ujasiri WANGU, karama ZANGU, kwa kuwa utapatana na pingamizi za uovu. Wale wanaofuata uovu, kuabudu Miungu nyingine na bado utashinda laana zao na Damu YANGU iliyomwagwa kwa ajili yenu pale Kalvari na neno la ushuhuda wako na neno la Ushuhuda WANGU.

Utakapopewa nguvu, nguvu ya JINA LANGU, Neno na Damu, tumia kushinda adui. Kemea maadui katika JINA LANGU. Usiwapuuze maadui kwa kuwa kuwapuuza inawasaidia kupata nguvu zaidi. Fichua maadui na hila za maadui na wewe utafanikiwa katika njia usizozijua.

Mpendwa WANGU, O Ninavyo hamu ya kukumbatia mikononi MWANGU na siku moja Nitafanya vivyo hivyo. Kwa kuwa unapohisi upweke ndipo Nipo karibu nawe kabisa. Ninasimama nawe unavyosimama kwa niaba YANGU. Milango ya jehanamu haitafaulu dhidi ya Kanisa LANGU. Nyinyi ni Kanisa LANGU. Mnapohisi kukataliwa na kusahauliwa ingawa hamwezi kuniona MIMI, mtajua Nipo hapo. Sitawaacha wala kuwatupa na Ninawapenda na upendo ambao hamna binadamu yeyote anayeweza kulinganisha. Ninawajua Watoto WANGU, Mashujaa WANGU na Bibi Arusi WANGU. Nyote ni haya yote na tena zaidi, Natabiri sasa kupitia huyu Handmaiden WANGU asiyejua ni yapi mengine atakayosema.

Ninawapeleka katika kiwango cha juu kushinda mlipokuwa hapo awali. Jitayarisheni, kwa kuwa adui anapowazunguka, jueni haya, ni kwa sababu adui anajua kuwa wewe sio wa dunia hii, lakini upo tu duniaini na mpo duniani humu kunitumikia MIMI, kufanya matakwa YANGU, Nikimwaga karama za RUACH ha KODESH WANGU juu yenu kwa wingi. Yote yaliyokuwa magumu hapo awali yatakuwa rahisi. Yote yaliyokuwa rahisi hapo awali mtafikiria kuwa yamekuwa magumu.

Lakini hii ni kwa sababu Ninawasongeza juu kushinda mlivyokuwa hapo awali. Nyie mtakuwa kama Petero na Nitasema, “Tupeni nyavu zenu ndani zaidi kwenye bahari,” na nyie mtasema “Lakini Baba sijawahi kufanya haya, au kuwa hapa.” Na Nitasema, “Lakini Mpendwa, samaki wapo kwa wingi kwa upande ule mwingine. Tupeni nyavu zenu kwenye upande ule mwingine. Nendeni kwenye maeneo ambapo hamjawahi kuenda bado. Msiogope, kwa kuwa MIMI Ndiye Mvuvi Mkuu. Ninajua ni chambo gani Nitakayotumia Ninapowatupa kwenye bahari. Nyie hamtarudi mikono mitupu. Niamini MIMI pekee na Nitawaongoza na kuwaelekeza kuwa hata wavuvi wakuu wa binadamu.

Yote aliyozungumza katika JINA LANGU yatakuja kufanyika. MIMI huwa sianzi kitu kizuri na kutomaliza. Huduma hii iliyokabidhiwa kwako leo hii itakua kwa kiwango kikubwa na mipaka. Jehanamu yote itatingizika kwa kuwa watakuona ukienda kwenye maeneo yao na kuchukua wafungwa na kuwaachilia huru katika JINA LANGU.

Someni Unabii huu kwa sauti ya juu, kwa nguvu haimo tu kwenye maneno yaliyoandikwa lakini pia maneno yaliyozungumzwa. Someni haya kwa wengine ili watasimama katika maelewano. Msishtuke kwa wivu na tamaa itakayojitokeza pande zote, kwa kuwa Ninafanya magamba kutoka kwenye macho yenu na yale yote mliyokataa kuyakubali mtayaona wazi, yale yote mliyokata kuyasikia, mtayasikia kwa uwazi.

Mpendwa WANGU jua haya, kila kitu kinachofanyika imepangwa na mikono ya Bwana. Ingawa itakaa kama maovu, Nitayageuza kwa mazuri. Hata mipango ya shetani, Nitayageuza na kuwakomboa nyote katika njia kuu. Watu lazima watakubali kuwa MUNGU unayemtumikia, YAHUSHUA ha MASHIACH bado anaongoza na kutawala na anaishi na hamna yeyote kama MIMI.

Mnapoomba, macho ya vipofu yataona, viziwi watasikia, waliofariki watafufuka tena, nafsi zitaokolewa, maadui wataanguka, kama vile tu Daudi alivyomshinda Goliathi. Maadui wataanguka kwa mkono WANGU pekee. Lakini Nitazungumza maneno ya kukemea watakapokuja dhidi yenu na laana zao. Mtasema, “MUNGU ninayemtumikia, YAHUSHUA ha MASHIACH ni mkuu kushinda maovu yoyote mtakayonifanyia, na YEYE husema kuwa hata nywele moja kichwani mwangu haitapotea kama sitaogopa na simwogopi binadamu yeyote au shetani kwa kuwa nimeshikilia funguo za Mbinguni, YAHUSHUA Ndiye Funguo hiyo Takatifu.”

Tabiri kwao haya, hivi ndivyo Asemavyo YAHUVEH wa Majeshi, “Itakuwa ni maadui watakaojitokeza dhidi yangu wanaosaka maisha yangu na kuangamiza huduma hii watakaoangamia. Kwa mkono wa MUNGU Anayeishi Anayesema msidanganyike MIMI sikejeliwi virahisi. Watavuna yote waliyopandilia. Lakini mtumishi WANGU hataangamia lakini ataishi kutangaza kazi ZANGU.” Hivi ndivyo Asemavyo YAHUVEH wa majeshi kwa kuwa ni jambo la kuogopesha kwa maadui WANGU kuanguka katika mikono ya MUNGU Anayeishi lakini kuna makazi na upendo kule kwa Wapendwa WANGU.

Fanyeni Nilivyowaamuru kufanya leo hii, kama Nilivyompa Binti YANGU maneno ya kusema kwenu Mpendwa WANGU na nendeni mbele na muwe na ushindi katika JINA la YAHUSHUA ha MASHIACH. Huduma ya Alpha na Omega Almightywind.

* * * * * * *

Ilipewa kwake Mtoto, Shujaa, Bibi Arusi wa YAHUSHUA Nabii Elijah (Elisheva Eliyahu) Tarehe 12/4/1997