Unabii 79: MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Nyinyi Watu, Hamwelewi!”

print

Unabii 79:

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Nyinyi Watu, Hamwelewi!”

Imeandikwa/Imezungumzwa katika Upako wa ROHO MTAKATIFU (RUACH HA KODESH)

Kupitia Mtume & Nabii Elisheva Eliyahu

Agosti 2, 2005 Saa 4:00 Alfajiri

* * * * * * *

Maoni ya Mhariri: Neno hili la Kinabii kutoka kwa YAHUVEH limeongezwa kwa sababu lilijenga msingi wa kiroho ambapo Maneno mengine zaidi ya Kinabii yakazungumziwa. Neno hili lilipozungumzwa, Upanga Unaokata wa YAHUVEH ulikuja juu ya wale wanaoheshimu Sabato YAKE ya Kweli Ijumaa Machweo hadi Jumamosi Machweo na wale ambao hawataki kuachilia Sabato ya mwanadamu ya Jumapili – siku ambayo Warumi wa zamani huabudu mungu wao wa jua.

Tarehe Agosti 1, 2005 Elisheva alikuwa anasikia, “MIMI, YAHUVEH, Nakuambia wewe Elisheva kuwaambia watu, ‘Nyinyi Watu, hamwelewi!” Tarehe Agosti 2, 2005 Elisheva alipokuwa akimwambia aliyekuwa meneja wa tovuti hii, Upako mkuu ukamjia na akaanza kuomba katika Ndimi Takatifu na Neno hili la Kinabii likaja.

* * * * * * *

Yafuatayo ni Unabii ulivyokuja

Na “Ndimi Takatifu” za Nabii Elisheva, kama ROHO wa MUNGU Anavyowajalia kunena (Matendo ya Mitume 2:3-4) lugha za mbinguni na duniani (1 Wakorintho 13:1). Elisheva huzungumza katika ndimi ikileta Unabii. (1 Wakorintho 14:6).

Inayo MAJINA ya KIEBRANIA ya MUNGU:

YAH/YAHU יה ni JINA TAKATIFU la MUNGU, kama vile “Alleluia” au “Hallelu YAH” הללויה ambayo humaanisha “Msifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH יהוה MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA יהושוע MWANA WA PEKEE WA MUNGU—(HA MASHIACH המשיח inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM אלוהים INAMAANISHA “MUNGU.”)

Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” שכניה תפארהkama JINA la KIBINAFSI la RUACH HA KODESH רוח הקדש, (katika Kiiengereza “ROHO MTAKATIFU”) —upo kwenye tovuti hii.

(HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania inamaanisha UWEPO WA MUNGU.)

Zaidi ya hayo, ABBA YAH אבא יה humaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH אמא יה humaanisha “MAMA YAH.”

Maandiko yaliyotajwa yametoka KJV au NKJV, isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo. Bonyeza kwa upande wa kulia zile nambari za maelezo ya chini (footnote) kufungua ukurasa mwingine.

* * * * * * *

Maneno ya YAHUVEH kwa Elisheva Aliyosema yaongezwe mbele ya Unabii zote:

Nilikuonya kitambo Elisheva, kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako.

Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako.

Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha.

Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.

Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli.

‘‘Mimi ndimi BWANA YAHUVEH: hilo ndilo JINA LANGU! Sitampa mwingine UTUKUFU WANGU, wala sanamu SIFA ZANGU.” Isaya 42:8

(Unabii 105)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:

Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

2 Mambo ya Nyakati 36:16

Alafu, Julai 2016:

Ole kwa yeyote atakayethubutu kujaribu kuwadhuru— hawa wawili walio na upako. Mtajuta kuzaliwa kwenu. Msiwaguse masihi WANGU, msiwadhuru Manabii WANGU (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22). Ingekuwa ni heri kwenu kama MIMI, ABBA YAHUVEH, ningerarua ndimi zenu!

(Unabii wa 128)

Na kutoka Nabii Ezra:

Nawaonya nyote—nyote mnaokuja dhidi ya Huduma hii NA UNABII hizi na Elisheva na Mimi, Wahudumu wa Huduma ya Amightywind—Nawaonya nyote sasa, Msiwaguse Masihi wa YAH, msiwadhuru Manabii WAKE’ (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22) kabla Ghadhabu za Gongo la YAH zije juu yenu. Lakini kwa wale waliobarikiwa na wao ni baraka katika Huduma hii, na ni waaminifu, na wamepokea Unabii hizi, baraka tele zitakuja juu yenu—yote kulinda yale ambayo ni ya YAH katika JINA la YAHUSHUA.

* * * * * * *

Unabii 79 Unaanza:

Agosti 2, 2005

Kama hamnitii MIMI sasa na kama mnapuuza ukweli sasa wa Siku Niliyoitenga kama Siku YANGU Takatifu ya Sabato— na kama hamfikirii ni muhimu kutii kila moja ya Amri ZANGU—ni nini kinachofanya mfikirie kuwa mtatii wakati wa Dhiki Kuu ijayo hivi punde?

Mbona ni rahisi sana kusikiliza mafunzo ya mwanadamu, wanapogeuza Maneno YANGU kufanana na mfano wa dhambi ya mwanadamu? Hata kama MWANA WANGU YAHUSHUA ni PUMZIKO lenu, YEYE sio Siku yenu ya Pumziko. MWANA WANGU YAHUSHUA SIO siku na Amri YANGU ya 4 inasema kwa uwazi kuitakasa, Siku YANGU ya Sabato ya Pumziko.

Ni yapi kati ya haya msiyoyaelewa? Ndio, pumzikeni katika YAHUSHUA. Kwa kuwa nira yake ni laini na mzigo WAKE ni mwepesi (Mathayo 11:30), lakini haya hayana uhusiano na Siku ya Sabato. Je, si YAHUSHUA alifuata Sabato?

Je, si Nilimtuma MWANA WANGU, YAHUSHUA, kuwa mfano kwenu? Hata mnajua ni kwa nini Niliitenga Siku hii ya Pumziko (Mwanzo 2:1-3)? Hamjui kuwa Siku hii ya Sabato yafaa kuwa Baraka kwenu na sio laana?

Amri YANGU ya Nne inasema kwa uwazi itakase Siku YANGU ya Sabato ya Pumziko. Je, si Sheria Niliyoiandika kwa Kidole CHANGU chenye Moto kwenye kibao cha mawe (Kutoka 31:18; Kumbukumbu la Torati 9:10) na Nikampa Musa kwenye Mlima Sinai husema, “Heshimu Siku YANGU ya Sabato na Kuitakasa” (Kutoka 20)?

Tena Ninawauliza, tangu lini MWANA WANGU, YAHUSHUA Akawa siku? Jiulizeni nyinyi wenyewe, kwa nini shetani alibadilisha siku ya Sabato kuwa Jumapili kama hakuwa anapanga kuitumia kwa madhumuni yake katika Dhiki Kuu?1 Msiwasikilize wale wanaohubiri mengineyo. Papa hapa ndipo ushindi ulipo.

Imeandikwa katika Neno LANGU Takatifu kuwa MIMI, YAHUVEH, siwezi kudanganya.

Mkinitii MIMI, kuna Baraka na ushindi kama ilivyosemwa katika Kumbukumbu la Torati 28. Kuna laana kwa wale hawataki kutii. Someni na kujifunza yaliyoandikwa katika Kutoka 31:12-17. Sabato ya kweli itakuwa ishara kati ya MIMI, YAHUVEH na watu WANGU, na itatumiwa kuwatambua wale wanaonitii MIMI kwa kweli na watakaonitumikia MIMI katika Dhiki Kuu.

Je, mtaniabudu MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA katika Sabato ya Kweli—Ijumaa Machweo hadi Jumamosi Machweo? Au katika Dhiki Kuu mtamtumikia na kumwabudu mwana wa shetani Jumapili?

Kama haufuati Siku YANGU Takatifu ya Sabato sasa, ni nini kinachofanya mfikirie kuwa mtayafanya haya wakati huo, katika Dhiki Kuu, ambayo haipo mbali?

Ndiposa Naongea kupitia huyu Ringmaiden WANGU ili onyo hili lisikike kote duniani. Je, hamjui wale wanaofunza kuwa haiwezekani kuwa mtiifu na kuwa Mtakatifu mbele YANGU hutoa visingizio kwa dhambi zao?

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Nyinyi watu, hamwelewi!”

Haya hayapo wazi kwa mjadala. Mtafanya yale ambayo MIMI, YAHUVEH, Nasema au katika Dhiki Kuu mtalipa na nafsi zenu. Wale waliojiinua na kusema, “Nitakuwa Hakimu wa Elisheva, Nitakuwa baraza la waamuzi wa Elisheva,” tubuni sasa hivi au mtaniona MIMI. Na Nitasema, “Ondokeni KWANGU, nyinyi mnaotenda maovu” (Mathayo 7:23; Luka 13:27), kwa kuwa MIMI ni YAHUVEH na MIMI sijihusishi kwa mjadala. MIMI PEKEE NI HAKIMU, MIMI PEKEE NI BARAZA LA WAAMUZI, MIMI PEKEE NI REFA.

Haya SIO maneno ya Elisheva.

Nyinyi wahubiri na manabii bandia wa uasi mnamshambulia. Mnamsema vibaya kwa Torah ambayo Niliiandika kwa kidole CHANGU. Mnawafunza kondoo na wanakondoo WANGU kuwa Ninapepesa macho kwa dhambi. Tubuni leo! Kwa kuwa MIMI NIKO sio MUNGU YAHUVEH Aliyebadilika kwa njia yoyote. Nyinyi mnaomhukumu, ondoeni boriti iliyomo machoni mwenu—kabla hamjajaribu kutoa kibanzi kilichomo machoni mwa mtu mwingine. Nyinyi mmechafuka kwa dhambi. Nyinyi mmechafuka kwa uasi. Nyinyi mmechafuka kwa kutotii. Nyinyi mmechafuka kwa kiburi.

Angukeni kwenye nyuso zenu mbele YANGU, kwa kuwa MIMI ni YAHUVEH MUUMBA wenu, ANAYEISHI MILELE. Mnathubutu kumlaumu MWANA WANGU, YAHUSHUA, kama kisingizio chenu kwa dhambi! Mnathubutu kukanyagia DAMU YAKE chini ya miguu yenu, mkitoa visingizio kwa dhambi zenu! Angukeni kwenu nyuso zenu mbele YANGU kabla haijapita mpaka na hakuna njia ya kurudi KWANGU (Waebrania 6:4-6)! Msimhuzunishe RUACH HA KODESH WANGU [ROHO MTAKATIFU]!

MWANA WANGU YAHUSHUA hakuja kuondoa Amri ZANGU.

MWANA WANGU YAHUSHUA Alikuja kutimiza Amri ZANGU. (Mathayo 5:17).

Muwe na shukrani kuwa MIMI siulizi tena mwajibike kwa amri 613. Mtawajibika tu kwa Amri Kumi na mnarusha mikono yenu juu na kusema, “Hizi ni nyingi kwangu.”

Mnapendelea kumsikiza mwanadamu anayebadilisha Amri ZANGU. Wanawaambia kuwaua watoto kwa tumbo wasio na hatia sio dhambi. Wanahalalisha kuavya mimba.

Wahubiri wanafunza katika kanisa zenu, “Msizungumze dhidi ya amri hii.” Kanisa zilizojipanga wanaokutana Jumapili wamechukua hongo kutoka kwa serikali za dunia hii. Wamechukua pepo ya hofu na kuivaa kama vazi.

Wako wapi Watumishi WANGU Watakatifu ambao hawajapuuza ukweli na bado huzungumza dhidi ya dhambi? Amri zenu za mwanadamu zinahalalisha yale ambayo MIMI Nilisema ni chukizo—wanaiita “ndoa ya jinsia moja.” Hata katika siku za sodoma na gomora hakukuwa na kitu kama “ndoa ya jinsia moja.” Hata katika siku za sodoma na gomora hakukuwa na dhambi kama hizi ingawa chukizo ya ushoga ilikuwemo. Lakini, hawakuthubutu kuiita ndoa!

Msiamini uongo unaofunza kuwa “unapookoka, unabaki daima kama umeokoka” (Ezekieli 33:12). MSIAMINI kuwa, kwa sababu YAHUSHUA Alilipa gharama pale Kalvari—sasa haijalishi—kuwa mnaweza kutenda dhambi, kuning’inia karibu sana na mpaka wa jehanamu mnavyotaka kwa sababu mmesema ombi la wokovu (Mathayo 7:21-23).

Mnafikiria kuwa si lazima kuweka matendo nyuma yake na bado mtaruhusiwa kuingia kwenye milango ya Mbinguni. Ondokeni KWANGU nyinyi mnaotenda maovu! Sitaki kusikia visingizio vyenu tena. Aidha mtakuwa Watakatifu au Nitawaambia, ‘Mnaotenda maovu, sikuwajua kamwe.’ 2

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Nyinyi watu, hamwelewi!”

Mnawasikiliza hawa wanadamu na kuketi kwenye kanisa zenu mkiamini uongo kuwa Jumapili ndio Sabato au haijalishi ni siku ipi iliyo Sabato. Mnaamini uongo ambazo wahubiri na rabi wengine wanafunza kuwa hakuna Nguvu za Upako kuu katika MAJINA YETU MATAKATIFU ya Kiebrania, YAHUVEH na YAHUSHUA na RUACH HA KODESH, kuwa jina lolote ni sawa.

Wahubiri wanawaambia kuwa si muhimu kujifunza Uyahudi wa MASIHI. Wanasema kuwa kama wewe sio Myahudi haikufai. Hawa wahubiri wa uasi wanafunza kuwa wewe ni taifa na sio lazima utii amri zilizopewa kwa Watoto wa Israeli. Je, mlisahau kuwa mlipomkubali MWANA WANGU, YAHUSHUA, kama MASIHI mkawa moja NAYE (Warumi 11:16-21)?

Mnashangaa, ‘Je, wapi Nguvu za Upako za Kanisa la Kwanza lililokuwa na ishara, maajabu na miujiza?’ Mnalia, “Wapi udhihirisho wa miujiza kama Siku za Kale?”

Rudini na mfanye yale Kanisa la Kwanza lilifanya na mtaiona miujiza hii tena. Kwa wale ambao hawajui, Ninasema kuwa mtawajibika tu kwa yale ambayo mliyoyajua. Sasa mtawajibika, pia kuwafunza wengine Kweli hizi. Lakini kwa wale wanaojua gani mazuri na hufanya mabaya, mtalipa na nafsi zenu.

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Nyinyi watu, hamwelewi!”

Mnatii hawa viongozi waovu wa kiroho wanaotoa visingizio sasa kwa dhambi. Ni nini kinachofanya mfikirie kuwa katika Dhiki Kuu hamtafanya haya tena—na mwana wa shetani?

Niliwaambia kupitia Unabii hizi Nilizoziachilia kupitia Elisheva kuwa MWANA WANGU YAHUSHUA Anarudi kwa Bibi Arusi WAKE Rosh HaShanah na itakuwa Sabato. Kama hamfunzwi sasa kufuata Sabato YANGU na Siku ZANGU Takatifu, na kujifunza MAJINA YETU MATAKATIFU na TORAH YANGU, je, mtajua vipi jinsi ya kuniheshimu MIMI na MWANA WANGU, YAHUSHUA, kama Nilivyokadiri? Mtajua vipi ni siku gani—bila kujifunza na kujionyesha kama waliokubalika—kuwa MIMI, YAHUVEH, Nimeitenga kuwa Sabato YANGU? Mtakuaje tayari YAHUSHUA Atakapokuja?

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Nyinyi watu, hamwelewi!”

Msipoheshimu na kufuata Sherehe ZANGU Takatifu, mtajuaje Rosh HaShanah ni nini na ipo wakati gani? Alafu, mtakapoachwa nyuma mtauliza, “Kwa nini?” Kwa hivyo Ninazungumza kupitia Ringmaiden WANGU na kuwaambia kabla ya wakati kuwa MIMI, YAHUVEH, Ninatabiri kupitia huyu Ringmaiden ambaye ni mmoja wa Bibi Arusi wa MWANA WANGU YAHUSHUA.

Bibi Arusi hawatabadilika tu katika miili yao ya utukufu—na kujazwa na UPAKO NI KAMA YAHUSHUA MWENYEWE ANATEMBEA NDANI YAO NA PAMOJA NAO—YEYE Atawajaza na UPAKO ambao HAKUNA chochote kitakachokuwa ngumu kwao!

Na kwa siku 40 Bibi Arusi wa MWANA WANGU YAHUSHUA wataonya, “Msichukue alama ya mnyama.” Wataenda kwa wale Niwaitao Wageni na kwa wale ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo na watawaambia, “Msitotii. Msipuuze ukweli, ingawa inaweza kumaanisha mpoteze maisha yenu.”

Mwaona, Ninatumia Ringmaiden huyu sasa, hata bila mwili wake wa utukufu, kama sauti iliayo onyo kabla ya wakati. Kwa kuwa Nimemwita yeye kuwa Nabii kwa wengi. Msichukue alama ya mnyama! Kuabudu Jumapili na alama ya mnyama ina uhusiano.

Jihadharini, mtapoteza nafsi zenu kama mtafuata Amri ya Kuabudu Jumapili wakati wa Dhiki Kuu. Itabidi Niwaombe msamaha Sodoma na Gomora, Niliowaangamiza kwa moto na sulfuri, Nitakaporuhusu hizi chukizo za dunia kuendelea zaidi ya ilivyo. Sitawaomba msamaha Sodoma na Gomora! Nitawaangamiza na kuwamaliza wote MIMI, YAHUVEH, Ninaowachukia.

Hawa wahubiri bandia wanatoa visingizio kwa dhambi na mmewasikiliza. Mnakuja kwa Huduma hii kwa Chakula chenu cha Kiroho: kuonja Upako, kunywa Maziwa ya Kiroho na kula Nyama ya Kiroho. Basi, ni wangapi kati yenu wanaopuuza ukweli na kuenda katika Kanisa za Jumapili? Mnaanguka kwenye miguu ya mchungaji wenu katika uaminifu. Na hapo ndipo mnapotoa fungu la kumi na sadaka zenu. Hamwezi kufaidika kwa njia zote.

Lazima mwamue ni siku ipi Niliyokadiri kama Sabato. Kwa kuwa kama Nilivyokadiri ni siku ipi iliyo Sabato, ni Siku ipi mnafaa kuniheshimu MIMI na kupumzika na kuja karibu NAMI—

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Nyinyi watu, hamwelewi!”

na pia mwana wa shetani ataamuru wale waliopuuza ukweli kumwabudu kwa siku atakayokadiri.

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Nyinyi watu, hamwelewi!”

Kama MWANA WANGU, YAHUSHUA, Alivyozungumza na YEYE Akasema ‘chukueni mvinyo na mkate huu, fanyeni hivi kwa ukumbusho WANGU’ (1 Wakorintho 11:23-26)—katika Dhiki Kuu ijayo, hamjui kuwa mwana wa shetani atawaambia wale watakaokubali alama yake, ‘Fanyeni hivi kwa ukumbusho WANGU’? Watakunywa damu ya waliouwawa kutoka kwa vikombe. Itajazwa na damu na kama mashetani (vampires), watakunywa hiyo damu.

Na kama vile sahani ya Ushirika inavyopitishwa—vivyo hivyo—watapitisha sahani na mwana wa shetani atasema, “Fanyeni hivi kwa ukumbusho WANGU’.” Nyama iliyochomwa ya waliouwawa watakula. Watakejeli Ushirika WANGU na Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Kwa kweli watachukia Bibi Arusi wa YAHUSHUA kwa kuwa wanajua maombi ya watakatifu ilimshikilia mwana wa shetani hadi wakati wa YAHUSHUA kuwaita Bibi Arusi wake. Maombi ya watakatifu yanafaa sana (Yakobo 5:16).

MIMI, YAHUVEH, Ninawaonya. Imeanza tayari.

Kutakuwa na mikutano ya ngono katika Kanisa za Jumapili katika Dhiki Kuu. Vivi hivi ndivyo mwana wa shetani atakavyowakejeli Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Kwa kuwa YAHUSHUA na Bibi Arusi WAKE ni moja, na WOTE wanaomwabudu YAHUSHUA, wanaomtii MWANA WANGU ni moja—kwa sababu ni uhusiano wa Kiroho wa mwili, akili, roho na nafsi—mwana wa shetani atakejeli wakati wa Dhiki Kuu: atapanga mikutano ya ngono katika Kanisa za Jumapili.

Mwanzo wa udanganyifu mkuu ni kanisa za mashoga. Tena Ninasema, dhambi hii imeanza tayari.

MIMI, YAHUVEH, Ninasema, “Nyinyi watu, hamwelewi!”

Hivi ndivyo Ninavyotumia Huduma hii, kuwatenga wanakondoo kutoka kwa mbuzi, kutenga ngano kutoka kwa magugu. Wale ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha MWANAKONDOO kabla ya Uumbaji wa Dunia hii, hawa ndio wale majina yao yatakayobaki kwenye Kitabu cha Uzima cha MWANAKONDOO. Hawatamwabudu shetani na watakataa alama ya mnyama, hata kama mmeyasikia haya au kuyasoma haya sasa na mwendelee kupuuza ukweli sasa, katika Dhiki Kuu mtafuata na kuheshimu Sabato ya kweli ambayo ni Ijumaa Machweo hadi Jumamosi Machweo ingawa itamaanisha maisha yenu na mtauwawa.

Majina yenu yameandikwa tayari kwa kuwa tayari Nilijua kabla hamjazaliwa katika dunia hii mtafanya nini. Msiposikiliza sasa, mtasikiliza wakati uo huo.

Wale wanaosoma na kusikia Ujumbe huu na kusaga meno yao kwa hasira kwa Ringmaiden WANGU, vivyo hivyo, mtasaga meno yenu kwa hasira na kukunja ngumi kwa, MIMI, YAHUVEH MUUMBA wenu katika Dhiki Kuu laana na mapigo yatakapokuja juu yenu moja baada ya nyingine na bado hamtatubu dhambi zenu. Kwa siku hiyo, kama jina lako lipo katika Kitabu cha Uzima cha MWANAKONDOO, Nitaifuta jina lako. (Ufunuo wa Yohana 3:5)

Vivyo hivyo, wote wanaoshangaa ni kwa nini Elisheva huyaleta haya juu yake, ni kwa sababu Ninatumia Huduma hii kuwatenga ngano kutoka kwa magugu—mnapoyasikia haya, mtajua kama nyinyi ni ngano au gugu. Je, wewe ni gugu la kuchomwa kwa HASIRA ZANGU, MOTO WANGU UTEKETEZAO? —ingawa MIMi [pia] humtumia sasa kulia kwa Bibi Arusi, kama sauti itakayolia kwa Bikira Watano wenye Hekima: “Msipuuze ukweli. Jitayarisheni. Kwa kuwa BWANA ARUSI wenu yuaja kwa Bibi Arusi WAKE katika siku ya Rosh HaShanah, Sabato.”

Bibi Arusi wa YAHUSHUA, pigeni magoti mbele YANGU. Mbaki Watakatifu na mbaki wanyenyekevu. Ombeni kuwa mtabaki kustahili kuwa Bibi Arusi wa MWANA WANGU YAHUSHUA waliofananishwa na Bikira Watano wenye Hekima, watakaonyakuliwa kwanza, inavyojulikana kama Mnyakuo (Rapture).

Wageni, ombeni kuwa mtakuwa katika Mnyakuo wa Pili ili muwe Wageni katika Karamu ya Arusi ya MWANAKONDOO.3 Wageni wamefananishwa na Bikira Watano Wajinga walioambiwa kuwa BWANA ARUSI Atawarudia tena baada ya Bibi Arusi wa YAHUSHUA kunyakuliwa.

Kwa hivyo tahadharini kwa sababu hamjui siku wala saa (Mathayo 25:1-13). Wakati MWANA WANGU Atakapokuja kuwanyakua Bikira Watano Wajinga—watakuwa wenye hekima.

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Nyinyi watu, hamwelewi!”

Je, mnajua ni nini kinachowatenga kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA au Mgeni? Ninawaambia sasa. Ni jinsi mnavyoitamani, jinsi mnavyoithibitisha kwa Utakatifu, upendo na kutii. Je, mpo tayari kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA, kufanya vitu njia YANGU na sio yako, mkimtumkuza YEYE katika kila mfanyacho?

Bibi Arusi wanajua kuwa wanafaa kufuata Siku ZANGU Takatifu. Bibi Arusi wanajua kuwa hawawezi kupuuza yale ambayo wanajua ni kweli. Wao ni wajasiri kwa kuzungumza Ukweli. Haya ndiyo yanamyotenga.

Ushirika pia ni kumbusho la Agano la Ndoa na YAHUSHUA. Bibi Arusi wa YAHUSHUA hutumia MAJINA YETU MATAKATIFU ya YAHUVEH na YAHUSHUA. Matamshi hayajalishi kwa kuwa Ninajua nyoyo zenu na hazioni aibu.

Je, una hamu kuu kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA? Je, una upendo kwake YAHUSHUA? Mnathibitisha vipi kuwa MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA, ni kwanza katika upendo wenu na maisha yenu na katika kila kitu mfanyacho? Haya ndiyo yanayokutenga kama Bibi Arusi wa YAHUSHUA, kwa kuwa Ninawaambia Siri: shauku na uzito wa upendo wako kwa YAHUSHUA ni ushahidi kwa wote kuona. Hii ndiyo ishara ya Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Wanahisi kuwa hawawezi kufanya ya kutosha KWANGU.

Sasa mnajua Siri. Mnaona wapendwa WANGU. Haya sio maneno yanayoweza kufichwa. Kwa kuwa Ninajua ni nani kwa kweli, kwa kweli, anaye hamu ya kulipa gharama ya kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Kwa kuwa sitamwita yeyote Bibi Arusi wa YAHUSHUA kama hawatakuwa na hamu hii. Kila siku Bibi Arusi wa YAHUSHUA huomba, “Nifanye niwe mtakatifu zaidi KWAKO.” Bibi Arusi wa YAHUSHUA ni mnyenyekevu na Mtakatifu mbele YANGU.

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Nyinyi watu, hamwelewi!”

Mbaki waaminifu KWANGU sasa. Msikuwe tu wasikizaji wa NENO LANGU lakini watendaji wa NENO TAKATIFU (Yakobo 1:22). Muwe Watakatifu kama MIMI NIKO Nilivyo Mtakatifu kwa kuwa ingawa upo katika dunia hii, hamfai kuwa kama dunia hii. Msiwaache wahubiri waovu kuwapoteza kondoo na wanakondoo WANGU, kwa wote lazima “watafute wokovu wao kwa kuogopa na kutetemeka” (Filemoni 2:12). Kwa kuwa “imani bila matendo haizai” (Yakobo 2:20).

MWANA WANGU YAHUSHUA Alifanya sehemu YAKE pale Kalvari. Sasa MIMI, YAHUVEH, Nasema kwenu, “Mfanye sehemu yenu”: Jitahidi kutii. Msifanye dhambi maksudi. Msitoe visingizio kwa dhambi. Msipokee maneno ya wahubiri wanaohubiri maovu.

Kwa kuwa MIMI, YAHUVEH, Nasema kwenu: Mbona mnamwita MWANA WANGU, YAHUSHUA, BWANA na hamtii YEYE? (Luka 6:46).

MIMI, YAHUVEH, Nasema, kama hamtatubu kwa njia mnazototii “Ondokeni KWANGU, nyinyi mnaotenda dhambi,” (Mathayo 7:23: Luka 13:27) [mtasikia] katika Siku ya Hukumu kwa kuwa sitavumilia nyinyi kukejeli DAMU TAKATIFU ya YAHUSHUA. Nyinyi mnaojiita “wahubiri,” wanaotoa visingizio kwa watu WANGU kutenda dhambi, TUBUNI leo kwa kuwapoteza kondoo na wanakondoo WANGU au MOTO WA PUMZI YANGU UTEKETEZAO, kama makapi katika UPEPO MKUU, utakubeba.

MIMI, YAHUVEH, Nasema kama haupendi Maneno haya yaliyozungumzwa kupitia Ringmaiden WANGU Elisheva, mtavuna matokeo. Kwa kuwa Nimekataa kujadili.

Kuna HAKIMU MMOJA tu. Kuna BARAZA LA WAAMUZI MOJA tu.

Na MIMI—YAHUVEH—MIMI Ndiye REFA wa PEKEE.

Kama haupendi Ujumbe huu wa Kinabii, msiipeleke kwake Elisheva, lakini ilete kwa MIMI, YAHUVEH. Yeye ni Mjumbe WANGU tu aliye na Upako.

Mwisho wa Unabii

Imezungumzwa, imeandikwa Agosti 2, 2005 Saa 4:00 Alfajiri kupitia huyu Ringmaiden wa YAHUVEH na YAHUSHUA kwa Sifa, Heshima na Utukufu WAO.

Ninabaki binti mnyenyekevu,

Mtume Elisheva Eliyahu

(Elisheva Eliyahu)

1

Danieli 7:25 Atanena maneno kinyume cha Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake Yeye Aliye Juu Sana, huku akijaribu kubadili sikukuu zao takatifu pamoja na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa [wakati, nyakati mbili na nusu wakati].

2

Mathayo 7:22-23; 25:41; Luka 13:25, 27; pia angalia Zaburi 6:8; Zaburi 119:115

3

Ufunuo wa Yohana 19:9 Ndipo yule malaika akaniambia, “Andika haya: ‘Wamebarikiwa wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo !’ ’’ Naye akaongeza kusema, “Haya ndiyo maneno ya kweli ya Mungu.’’