133 NDOTO YA KINABII YA MTOTO MCHANGA ALIYE NA NJAA!

print

UNABII 133

NDOTO YA KINABII YA MTOTO MCHANGA ALIYE NA NJAA!

Umeandikwa/Umesemwa chini ya Upako wa ROHO MTAKATIFU (RUACH HA KODESH)

Kupitia Mtume & Nabii Elisheva Eliyahu

Ulipokelewa Desemba 19, 2001 – Uliachiliwa tena May 10, 2010

 

Huu ni unukuzi:

Nabii huona vitu mapema. YAH huonya daima kupitia Manabii WAKE wa ukweli. Na nilikuwa na hii ndoto, ndoto dhahiri saana—ambayo YAH Ananiambia nionye [nayo]—na hiyo ilikuwa Desemba 19, 2001. Na sababu ninashiriki hii sio kufanyiza hofu, bali kuuliza maombi yenu kwamba hii ndoto HAitatukia!

Katika wakati wa hii ndoto [katika 2001], ilikuwa ni DHARURA na ilionekana kama ilikuwa inaenda kufanyika Marekani. Sisi tunaoamini katika YAHUSHUA, tuna ‘ulinzi wa kijeshi’ lenye uweza mkubwa ambalo linatoka moja kwa moja kutoka Mbinguni na ni jeshi la malaika, malaika wapigaji vita. Na ABBA YAHUVEH pekee Ataweza kutuonyesha rehema zaidi kwa sababu wakati hii itafanyika, kile hii ndoto inaenda kueleza, ni shambulizi la nyuklia!

Na katika Unabii wa mwisho ambao nilipewa ambao utatundikwa hivi karibuni, unaonya—na pia katika Unabii wa Donald Trump ulionya (131, Donald Trump ni kama Bisi Ikichanua!).

Kuna shindano la kuona ni nani anaenda kufinya hicho kitufe,hicho kitufe chekundu. Kwa sababu yeyote atakayefanya, haya, ni shambulizi la nyuklia. Na kutakuwa na kulipiza kisasi.

Hivyo naita hii ndoto, “Ndoto ya Mtoto Mchanga Aliye na Njaa.”

Ndoto Inaanza

Nilikuwa nimesimama nje nikiangalia anga nzuri ya bluu. Yote yalikuwa na amani. Nilipokuwa nikiangalia juu, niliona miviringo 4 angani ikichorwa ni kama Kidole cha MUNGU YAHUVEH kilikuwa kinaichora polepole sana. Mviringo wa nne ulipochorwa, nilisikia kelele ya mgurumo mkubwa. Nikaingia ndani ya nyumba, na upepo MKUBWA ulikuja ukiharibu na kuua. Ilikuwa ni mlipuko wa nyuklia, kama kutokana na athari za bomu ya nyuklia! Nilitazama katika hofu yale maafa na uharibifu.

Katika nyumba yangu, niliona mwanamke na kitoto kidogo mikononi mwake. Niliangalia kitoto. Na kilionekana kama kimekufa na kuwa na utapiamlo sana. Na nikamwambia yule mwanamke, mamake, “Mbona hukumlisha mtoto?”

Na akaniangalia kwa ubaridi na kusema, “Kwa sababu mtoto amefunga.”

Halafu kabla nikichukue kitoto kutoka kwake, alifungua dirisha na kukitupa nje [kutoka] dirisha la ghorofa ya 2. Nilikimbia nje katika ule mnururisho na upepo wa kuharibu, na kukishika kitoto mikononi mwangu, na kitoto kikaanza kupumua tena!

Nilipokuwa nimesamama pale mwanaume alikuja kwangu—na alikuwa ananipita tu—uso wake ulikuwa umechomwa sana kutokana na mnururisho wa ule mlipuko wa nyuklia, na ulikuwa mwekundu na kiwango cha tatu cha kuchomwa au mbaya zaidi. Hakusema kamwe neno moja. Aliendelea tu kutembea na kunipita.

Nilirudi ndani ya nyumba yangu, nikiwa nimelindwa kabisa kutokana na mnururisho kwa sababu nilijua hakuna chochote kingendhuru—pamoja na kitoto. Na nikakilisha kitoto maziwa kutoka kwenye chupa.

Baada ya muda zile upepo za kuharibu zilisimama. Yote yalionekana kuwa na amani. Halafu nikaangalia anga tena, na nikaona mviringo wa kwanza ukianza, nilianza kupaaza sauti, “TUBUNI na mgeuzie mioyo yenu YAHUSHUA! Kwa maana tena hukumu imekuja!”

Wachache sana walisikiza. Niliona ile miviringo nyingine 3 yote katika safu—4 kwa jumla.

Kisha sauti ya mgurumo ambao siwezi kueleza. Halafu ule upepo wa kuharibu ukaja tena. Na ulikuwa mlipuko wa nyukilia mwingine ambao ulitokea!

Mwisho wa Ndoto

Hapa ndipo tulipo. Na tunaomba tu kwamba tuwe na muda zaidi wa kufikia nafsi zaidi. Na katika hii ndoto, nilikuwa na mwili uliotukuzwa wa aina fulani, kwa sababu huo mnururisho, sikuogopa—milipuko, upepo. Nilikuwa katika mwili uliotukuzwa.

Pia ni—wakati YAH Anapeana maono, ndoto, unabii, kunaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Na hivyo, natambua pia kwamba hii inaweza kuwa na maana mbili. Maana tunajua shambulizi la nyuklia litatukia. Ni jambo la muda tu!

Yule mwanamke ni dini. Na kitoto ni mikusanyiko ya waumini. Dini ya utaratibu na kanisa za utaratibu zinakosesha watu chakula cha kiroho: zikiwalazimisha wafunge kwa ajili ya maarifa zaidi ya kiroho na ukweli za kinabii na mafunuo; kanisa nyingi hata hazitaruhusu Nabii kuagua.

Yule mchungaji atauliza huyo mtu kabla ya huo wakati, “Kabla unaweza agua, nataka nione…” Wanawaambia haya, “Nataka nione kile unaenda kusema.” Hilo haliwezekani kwa Nabii wa ukweli!

Nabii wa ukweli anafungua tu mdomo wake na ABBA YAH, YAHUSHUA WAnanena! Ni wale wa bandia tu wanaweza fanya hivo [kuonyesha kabla ya wakati]. Na ninatumika, nimetumika kulisha wale watu ambao wamekoseshwa chakula, na bado wanaenda kwa kanisa zao—kwa kuenda miaka 22 kwenye mtandao ikija Aprili 4, 2017.

Na wachungaji wanatoa dhabihu watu kwa ajili ya kujilisha wenyewe, utajiri na udhibiti. Na wanafikiria wao WANAMILIKI KONDOO, (watu, kusanyiko la waumini)! Na wataishi katika makasri, na kuendesha Mercedes [Mabenzi], [ma]Rolls Royce! Wanakuwa na jeti, jeti zao za binafsi! Na kutowahi hata miliki tu kasri moja, lakini kwa kawaida nyingi!

Na wanasahau kuwa kuna tu MCHUNGAJI MMOJA MZURI. Na ni YAHUSHUA HA MASHIACH (AMBAYE wengine sasa wanamwita YESU KRISTO)! Tafadhali onya kila mtu!

YAHUVEH Aliniongelesha katika hiyo ndoto na kunionya kwa nini Atainua [ondoa] ua lake la ulinzi tena, na ni kwa sababu hata wapagani wanaabudu mungu wa kipagani, lakini ni nani kweli Marekani wanaabudu? Ni mungu yupi nchi yoyote duniani inaabudu? Wayahudi wanaabudu ABBA YAH, YAHUVEH. Wana ‘majina’ mengi [wanayoMwita]: HaShem, Adonai, lakini ninaMwita kwa JINA LAKE YAHUVEH!

Ndoto Inaanza:

Katika Novemba (tena ya 2001), nilikuwa na ndoto kama hiyo.Nilikuwa nikitembea kwenye barabara na ng’ombe aliyejaa maziwa alinifuata popote nilienda. Na hata hakuwa ng’ombe wangu. Mkulima alinishtaki kwa kumuibia ng’ombe wake! Nilisema singeweza komesha ng’ombe aache kunifuata, ilikuwa ni chaguo lake!

Niliona miraba 3 katika mstari ikichorwa na Kidole cha YAHUVEH katika anga. Nilisikia sauti kama mgurumo ambao siwezi eleza. Ili, ilikuwa … ni yenye sauti kubwa!

Halafu niliona—niko kwenye milima na mawe makubwa yalikuwa yanaelekea kule nilikuwa. Nilikimbilia bahari kule nyumba yangu ilikuwa kwenye ndoto. Niliingia katika nyumba na halafu nikaona hizo miraba 3 tena ikiwa inachorwa katika anga. Niliangalia katika hofu, na nilijaribu kufikiria ni njia ipi ya kufa ilikuwa na uchungu mdogo kabisa.

Maana nilidhani bahari ingefunika nyumba na wote wangezama majini kama ningebaki.

Kwa hivyo niliamua kuenda kwenye milima tena. Nilisikia ule mgurumo. Na punde mraba wa 3 ulichorwa, niliona—kabla ningeweza hata kusonga—fataki angani. Na ya kwanza, rangi zisizoiva, zilikuwa zile za kuchosha wakati fataki huanza. Halafu fataki za rangi zenye kung’aa! Na zilikuwa fataki za kupendeza. Sikukimbia, nilizitazama tu zile fataki.

Mwisho wa Ndoto

Ningependa kujua utambuzi wa hizi ndoto.

Najua hao ng’ombe ni watu waliojaa maziwa, wana maziwa ya Neno. Lakini wanahitaji zaidi. Wanahitaji nyama ya kiroho. Ni sala za bidii za watu wema pekee zitakazo leta mengi (Yak 5:16). “Kama watu wangu” wataanguka kwenye nyuso zao na “kunyenyekea […] NItasikia [maombi yao] … na kuponya nchi yao” (2 Nya 7:14)! Tafadhali chukueni hizi ndoto kwa uzito.

Kile kitu kimoja kizuri ni kama wewe ni mali ya ABBA YAHUVEH & YAHUSHUA, unaweza simama juu ya Maandiko ya Zaburi 91, kwamba Atakuficha chini ya Mabawa YAKE: Mahali pa Siri pa MUNGU ALIYE JUU KABISA, kama ilivyotamkwa katika Zaburi 91!

Je, kunacho chochote kigumu kwa YAH?

Wale watoto 3 Waebrania (Dan 3) walitupwa kwenye tanuri ya moto iliyotiwa joto mara 7 zaidi na hakuna kilichochomwa bali zile kamba zilizotumiwa kufunga mikono na miguu yao. YAHUVEH Anaweza tuepusha na madhara wakati huu pia! Hata miili yao haikunuka moshi! Kwa hivyo kile napaswa kusema ni tunajua hili linaenda kufanyika.

Na kwa wale ambao ni Bi-arusi wa YAHUSHUA, wata aidha kuwa katika miili iliyotukuzwa au watakuwa Mbinguni.

Ninaomba katika JINA LA YAHUSHUA kwamba mchukulie hizi ndoto kwa uzito. Donald Trump ametangazwa kama Rais wa pili. Yeye si mchochezi wa vita; Putin anataka kufanya amani na Marekani. Nilipewa Unabii kuhusu Donald Trump (Unabii 131, Donald Trump, Anachanika kama Bisi!) Na hii Huduma [AmightyWind]—hii Huduma ya Wayahudi wa Kimesaniki—tuliambiwa kuomba kwamba Donald Trump atakuwa Rais. Na MSIFU YAHUSHUA yeye ni [Rais]!