134 MIMI, YAHUSHUA NAKUPELEKA KWENYE MWINUKO MPYA WA IMANI YAKO!

print

UNABII 134

MIMI, YAHUSHUA NAKUPELEKA KWENYE MWINUKO MPYA WA IMANI YAKO!

Unabii Uliopotea Umepatikana!

Umesemwa chini ya Upako wa RUACH HA KODESH

kupitia Mtume Elisheva Eliyahu

Ulipokelewa Hanukkah Desemba 11, 2008

Umeachiliwa tena Mei 10, 2017

 

Ingawa sehemu za ujumbe huu ni Neno [kwa] mtu binafsi, zengine zinahusu wafuasi waaminifu wote wa YAHUSHUA. Tunaomba mbarikiwe nao!

Hii ilirekodiwa kwenye tepu ya sauti. Huu ndio unukuzi [wake]:

 

Elisheva: Tulipokuwa tukiomba baada ya ushirika mtakatifu, kwamba Ulikuwa na mambo Ulikuwa Unataka kusema na tulikuwa tunaKUshukuru kwa kila kitu na kuKUletea mahusiano yetu yote.

Kwa hivyo kwanza ninakukemea na kukufunga wewe shetani na wana falme wote, mamlaka, mahimaya, wakuu katika sehemu za juu, sehemu za chini, sehemu za giza na juu ya haya maji ya bahari katika JINA la MPENDWA wetu YAHUSHUA MASHIACH—umefungwa, hautahusiana na sehemu yoyote ya huu wakati wa maombi—hauwezi hata sikia kile ninaenda kusema kwa sababu hauna haki juu yangu shetani, masikio ya mapepo wako yamefanywa viziwi na macho yenu kufanywa vipofu. Na yeyote mwingine anayetafuta kudukiza, ABBA YAHUVEH, tunaKUshukuru kwa kuharibu vifaa vyao! Kwa yeyote anayeangalia kwa mbali ninaKUuliza Ung’oe macho yao. Hawaendi kusikia. Hawaendi kuona. Kwa maana hawastahili kutusikia tukiomba kwa BABA wetu YAHUVEH, katika JINA la MPENDWA wetu YAHUSHUA.

Hivyo sasa ninaKUuliza tumetokea shiriki tu ushirika mtakatifu wetu, ninaKUuliza Uitie mafuta midomo hii, ulimi na Usiwache neno moja litoke ambalo si LAKO. Nimeamini daima katika imani kuwa WEWE haUngeruhusu itokee na katika uaminifu WAKO, katika upendo WAKO na rehema YAKO, haUjaruhusu. Hii ni midomo YAKO. Uliitengeneza. Tafadhali zungumza kuipitia sasa, katika JINA LA YAHUSHUA, MASHIACH MPENDWA, tunaomba. Ni nini iko juu ya Moyo WAKO MPENDWA YAHUSHUA? [Ndimi Takatifu]

Unabii Unaanza

Sasa watoto WANGU NInapeleka imani yenu kwenye kiwango kipya. Jione kwenye eleveta. Jione pale ulianza mara ya kwanza. Na unapozidi kukaribia Mbinguni, Ninakupeleka kwenye ghorofa mpya, mwinuko mpya wa imani yako. NInafunza kila mmoja wenu. MIMI NI MWALIMU BINAFSI WENU. Kila mmoja wenu ana Sikio LANGU, ana Jicho LANGU. Kile mnafaa mfanye ni kusalimisha maisha yenu KWANGU na kusema, “Sitaki kufanya hili njia yangu.”

Najua kila moja ya woga zenu. Hamwezi NIficha, kwa hivyo ni heri mkiri ili NIweze kuondoa huo woga. Hakuna aibu katika woga ila ukikuzuia kufanya kile NImekuambia ufanye. Hakuna aibu katika huzuni, ila ukikuzuia kufanya kile NImekuambia ufanye.

NImewapa nyote kazi zenu. Mnaziita “kazi”. MIMI NInauita “mwito”. Lakini NImeweka mipango kama ramani ya maisha yako. Wengine wenu hamwezi bado ona ramani vizuri. Inachukua mtu stadi kusoma ramani.

Lakini kupitia imani yako utaweza kusoma hiyo ramani. Kupitia imani yako utaweza kusikia sauti YANGU. Kupitia imani yako utaweza kuona kupitia macho YANGU. Kwa maana hakuna sadaka unayoitoa kwa Utukufu WANGU-[ambayo] inavyopatikana kuNIpendeza kama harufu nzuri kwenye Mapua YANGU, utazawadiwa. Hii zawadi itakufuata hadi mbinguni.

Kuna wale ambao watafika tu Mbinguni na pumzi yao ya mwisho ya kufa. Lakini Bi-arusi WANGU hauhesabiwi miongoni mwao. Unazo zawadi zinazokufuata, kwa maana unaNItumikia kwa uaminifu sana.

Hii Hanukkah unafurahia maadamu umefunzwa kuwa ni [wakati] NIlitungwa kama mimba. MIMI sie YAHUSHUA wako, MASHIACH wako, NURU yako ya KUKUONGOZA?

Wayahudi wa Kiorthodoksi wanasherekea Sherehe ya Nuru na hata hawaelewi wanasherekea MIMI NILIVYO. Waambie Elisheva. Acha hii Huduma ipaaze kwa sauti kubwa na wazi! Ilikuwa ni zaidi ya taa ya mafuta ambayo haikuzima. MIMI NDIYE hiyo TAA YA MAFUTA INAYOISHI! MIMI NDIYE MAFUTA YANAYOISHI! Na hakuna mtu anayeweza kuchukua maisha YANGU! NIliyaweka chini kwa hiari na NIkayachukua tena na NIkaishi tena.

NImekupa ufunuo. Hii huduma imeusema na itaendelea kuusema: NInastahiwa kuwa mnataka kusherekea kuzaliwa KWANGU hapa duniani na NIliwaambia hiyo ilikuwa wakati wa Sukkot. Wafunze.

NIliinua YDS [Mashujaa wa YAHUSHUA], wale ambao wanabeba JINA LANGU, ‘Mashujaa wa YAHUSHUA’. Kwa sababu ni mtandao, hauwezi sema sababu ya kwa nini lakini unapswa kuwaita wakusanyike katika maombi, hasa wakikufunika wewe [Nabii, maombi ya kulinda] kwenye hizo siku.

Ni muhimu kuwa wafunge na waombe kwa wale NInaowaongoza kufanya hivyo.

Kwa maana NImeweka huduma hii kwenye mtandao na Neno LANGU litaenda katika vitabu vilivyojalidiwa vigumu […]

Enyi wapenzi WANGU! Weka imani yenu ndani YANGU. NIruhusu NIwapanue katika njia hamjapanuliwa bado.

Ee jinsi NInavyokupenda […]! Ee jinsi NInavyotamani sana Bi-arusi WANGU. NIngekutolea kasri ya madola bilioni kwenye hii dunia na kama ingekuwa chaguo lako, ungesema, “Unaweza iweka YAHUSHUA! Ninataka tu kasri yangu ya Mbinguni ili kuona Uso WAKO, kutembea kwenye barabara za dhahabu, kuzungukwa na Utakatifu.”

Vumilieni watoto WANGU! Vumilieni watoto WANGU kwa muda kidogo tu! Vumilieni watoto WANGU wachanga! Vumilia Bi-arusi WANGU! Sio mbali sasa utakuwa kando YANGU! Fanya tu NIlichokuita ufanye kwa maana muda u mfupi zaidi ya fupi! Endelea kulisha kondoo na wanakondoo WANGU ili wasipotee.

[…] Unashangaa pale unaenda kupata muda huu wote. NIruhusu NIkupe huo mpango. Nyinyi nyote NAwaambia hili, usianguke kwenye dhambi ya dhana na kudhani unajua kile NInafanya.

Kuna kitu kimoja utajua, mipango NImekutengenezea ni za wema wako na SItaruhusu uovu ukushike. […]

NIshakuambia, Adam, tia mafuta nyumba, sio ndani pekee bali pia nje na tia mafuta [kwenye] njia ya binafsi ya kuingia nyumbani. Ichukulie kwa uzito; usipuuze kutia mafuta kwa nyumba. Adam, hii isiwahi koma! Hii ni silaha umepewa. Hii inazuia adui nje. Mwaga mafuta kidogo kwenye hiyo njia ya binafsi ya kuingia nyumbani. Hili ni funzo mpya NInakupa na uliza vikosi VYANGU vya malaika Watakatifu kuzunguka na kulinda nyumba.

Adam, endelea kulisha kondoo na wanakondoo WANGU kwa maana Poland ni moto wa nyikani ambao haujawahi zima. Wakati tu utakapofika Mbinguni Adam utaona jinsi kazi yako ya bidii imezaa matunda, wakati mmoja wa Mpolandi baada ya mwingine watakuja kibinafsi na wakuambie. Adam, ee Adam, unanipendeza sana MIMI. Na NInalinda upendo wako Adam, ee kwa wivu sana. Kathrynyah, ee, Kathrynyah, unaNIpendeza sana MIMI na NInalinda wakati wetu pamoja kwa wivu saana.

 

Mwisho wa Neno

 

Elisheva: Asante. Vidole vyangu vimeganda! Hayo ndiyo yote ninasikia! Asifiwe YAHUSHUA, ABBA YAHUVEH! Hallelujah MPENDWA RUACH HA KODESH! Asante. Asante. Asante.

Hivyo umesemwa na kuandikwa

kupitia mtoto, shujaa wa YAHUSHUA,

Elisheva Eliyahu

Hanukkah 2008