30 TAHADHARI! NITAFANYA MSICHOFIKIRIA, KWA WAKATI MSIOFIKIRIA, KATIKA NJIA MSIOFIKIRIA!

print

UNABII 30

TAHADHARI! NITAFANYA MSICHOFIKIRIA,

KWA WAKATI MSIOFIKIRIA,

KATIKA NJIA MSIOFIKIRIA!

UMEPEWA MTUME ELISABETH SHERRIE ELIJAH (ELISHEVA ELIYAHU)

FEBRUARI 8, 1999

 

Hii inatoka Unabii 105, YAHUVEH Alisema ujumbe huu uwekwe katika kila Unabii kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisheva(Elisheva) kutoita Huduma baada ya jina la mwanaume au mwanamke hata kabla kuwepo na huduma. Niliweka ndani ya roho yako kwa kuwa hakuna lolote kwa haya ambalo limefanyika kwa mkono wako, hakuna lolote kwa haya ambalo limetoka kwenye kinywa chako. Limetoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH ambaYE amezaa. Limetoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako ambaYE amezaa. Limetoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako ambaYE amezaa. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa upepo wa SH’KHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, Upepo Takatifu wa Uamsho, sio kwa pumzi yako au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Julai 2010 MUNGU YAHUVEH pia alisema yaongezwe haya kutoka Mambo ya Nyakati ya 2 kabla ya kila Unabii:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”


Unabii Unaanza

Moyo wa mtu utavunjika na hofu wakitazama kinachokuja juu ya hii dunia katika mwaka wa 2000 na kuendelea. Kwa sababu wale wanaodhihaki wale wanaoonya, mtaonja yale yatakayokuja. Tahadhari, kwa maana usipuuze rehema YANGU, usikanyagie Damu ya MWANANGU chini ya miguu yako, kuifanya isiwe takatifu, ukitenda dhambi na kusema, “Nimesamehewa.” Kwa maana Nawaambia hakuna msamaha kwa kufanya hivi. Tahadhirini kwa wale wanaofikiria MIMI ni Mungu wa kudhihaki! Tahadharini na wale wanaochukulia upendo na rehema na uvumilivu WANGU kama kawaida. Tahadharini na wale wanaosema,”Kisasi sio changu asema Mungu wa usawa, upendo na vita vyote viwili.”

Hii dunia itavuna kile imepanda. Watoto Wachanga, Bi-arusi, Wachaguliwa, na Wateule WANGU wanaoishi takatifu ni kama hizi ni siku za mwisho na kuNItukuza kwenye Sabato ya Ukweli na Kuitakasa, wanaNItazamia, NItarudi na kupata Bi-arusi WANGU ana mafuta katika taa yake, na akingojea Bwana Arusi wake, Mwokozi wake. NItamchukua kama Bi-arusi WANGU. Lakini wale ambao wanayo taa pekee na hawana mafuta watapata wana mfano wa umungu kwa nje na hakuna umungu kwa ndani. Wataenda na kuNItafuta na SItapatikana.

Hakuna anayeweza sema hawajaonywa siku hii.


Hivyo umesemwa, Hivyo umeandikwa siku hii umepewa Mchungaji Elisheva Elisheva Eliyahu 2/8/99